My Items

I'm a title. ​Click here to edit me.

Dereva wa maisha yako ni wewe mwenyewe

Kuanzia sasa dereva wa maisha yako ni wewe mwenyewe bila kujali mto ulikugharikisha na kukuleta katika wakati mgumu kimaisha, unaweza kuuelekeza mto wako utitirike kuelekea uelekeo unaoutaka wewe.

Karibu na wewe usimulie stori yako

Karibu na wewe mpendwa, usimulie kuhusu maisha yako ili uwe huru kutoka kwenye uchungu na visasi maana kusimulia kwa mtu unayemwamini ndiyo namna pekee ya kunusuru maisha yako yanayoendelea.

Chukua hatua na ubadilishe mwelekeo wa maisha yako

Natamani kumwambia mtu anayehangaika sasa hivi kwamba - unapendwa, una thamani kubwa, haya magumu yatapita.

Ningemkumbatia na kumpa moyo kwamba leo anaweza kuchukua hatua kubadilisha mwelekeo wa maisha yake.

Kilichopita kimepita, kilicho mbele kipo mikononi mwetu.

Kila mwanadamu ana changamoto zake

Sisi tulipata nafasi ya kusimulia kuhusu maisha yetu, sasa tupo huru!

Nilipokuwa RLabs, niliogopa kusimulia maisha yangu, nilivyopata ujasiri wa kusimulia, nilijisikia huru.

Mimi niligundua sikuwa peke yangu, wengi wamekuwa na changamoto, lakini huwezi kujua.

Ni ngumu kuboresha maisha unapokuwa na mawazo mengi na majuto

"Duh! Watu wanapitia magumu sana. Inasikitisha, hasa mtu anapopoteza matumaini au kujisikia kama yuko peke yake.

Ni ngumu sana kuboresha maisha unapokuwa na mawazo mengi na majuto. Au kama watu wamekushusha thamani na kukuambia haufai.

0657 893 866

  • Instagram
  • Facebook
  • Twitter

©2020 by RLabs Tanzania. Proudly created with Wix.com